Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Utawala haram wa Kizayuni hivi sasa unaomba Msaada Marekani iwasaidie kuingilia vita yake dhidi ya Iran baada ya wao kuanzisha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kupokea jibu Kali la kusaga meno kutoka na Makombora hatari ya Iran yanayotua kila wakati katika Maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kimabavu na Israel.
Kumbuka yote hayo yanakuja baada ya Israel kuanza uchokozi wake dhidi ya Iran, na sasa maji yamewafika shingoni, Moto wa Iran ni mkubwa tofauti na walivyotarajia katika mahesabu yao. Iran imeapa kuwapa kipigo cha onyo kama hatua ya kwanza, na kisha kipigo cha kuumiza na kutia maumivu katika hatua ya pili.
Your Comment